Pages

Sunday, August 7, 2016

UMRI NI NAMBA TU,IBRAHIMOVIC APELEKA UBINGWA MANCHESTER UNITED


Na: Daniel Fute

Bado atasimama katika mstari wake ule ule wa kwamba "Umri ni namba tu kama namba nyingine" hivi ndivyo alivyo tudhihirishia rasmi Zlatan Ibrahimovic katika mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu ya England katika kombe la Ngao ya Jamii.

Goli la Ibrahimovic alilofunga katika dakika ya "83 limekuwa goli bora sana kwa klabu ya Manchester United na kuifanya klabu hii kuzidi kujiandikia rekodi katika michuano hii ya Ngao ya jamii.

Magoli ya Manchester United yalifungwa na Jesse Lingard pamoja na Zlatan Ibrahimovic, wakati goli la Leicester City likifungwa na Jamie Vardy.


No comments:

Post a Comment