Hii ni Blog ya michezo ambayo inahusu sana mchezo wa soka, Hapa utaweza kupata habari mbalimbali za Soka katika kila sehemu duniani. Tangaza nasi kupitia 0713875490/0625557298
Hii ni Blog ya michezo ambayo inahusu sana mchezo wa soka, Hapa utaweza kupata habari mbalimbali za Soka katika kila sehemu duniani. Tangaza nasi kupitia 0713875490/0625557298
Pages
▼
Monday, August 8, 2016
SIMBA WA KATA KEKI KWA USHINDI WA GOLI NNE DHIDI YA AFC LEOPARDS
Na: Daniel Fute
Mabadiliko! Mabadiliko! Mabadiliko! Ni kweli Simba walikuwa wanahitaji hili neno lifanyike msimu huu katika timu yao na kama isingekuwa hivi si dhani kama klabu hii ingepata kile ambacho wanachama na mashabiki wengi wa Simba walikuwa wanakitaka.
Leo klabu hii imeadhimisha miaka 80 na pia leo hii ilikuwa siku yao ile maalumu ya 'Simba Day' ambapo siku hii ilianza rasmi mwaka 2009 kwa kujumuisha vitu vingi kuhusu klabu hii ikiwa kama Utambulisho wa jezi mpya,Utambulisho wa Wachezaji na pia hata kufanya kitu katika jamii.
Vile vile siku hii ya 'Simba Day' klabu hii ya Simba hualika klabu yeyote inayotoka nje ya Tanzania kwaajili ya kukipimisha kikosi chao kipya,na mwaka huu Simba wameweza kuwaalika klabu ya Afc Leopards kutoka Kenya kwaajili ya kuadhimisha siku yao leo hii.
Katika Mchezo uliopigwa uwanja wa Taifa jioni ya leo klabu ya Simba imeweza kuwafunga Afc Leopards magoli 4 kwa 0,Magoli ya Simba yalifungwa na Ibrahim Ajib aliyefunga magoli mawili, Shiza Kichuya na Laudit Mavugo.
Uwezo waliouonyesha Simba katika mchezo huu dhidi ya Afc Leopards inaonekana dhahiri klabu hii imebadilika na wana kitu wana kihitaji katika msimu mpya wa Ligi kuu ya Vodacom achilia mbali uwezo wa wachezaji mmoja mmoja ambao wameonyesha kiwango cha juu kwaajili ya shauku ya kujihimarishia nafasi zao chini ya kocha Joseph Omog.
No comments:
Post a Comment