Hii ni Blog ya michezo ambayo inahusu sana mchezo wa soka, Hapa utaweza kupata habari mbalimbali za Soka katika kila sehemu duniani. Tangaza nasi kupitia 0713875490/0625557298
Hii ni Blog ya michezo ambayo inahusu sana mchezo wa soka, Hapa utaweza kupata habari mbalimbali za Soka katika kila sehemu duniani. Tangaza nasi kupitia 0713875490/0625557298
Pages
▼
Tuesday, August 9, 2016
USAJILI WA POGBA WA WATUPA MBALI AKINA DI MARIA NA MARTIAL KATIKA KLABU YA MANCHESTER UNITED
Na: Daniel Fute
Pesa ndio sabuni ya roho na Pesa ndio adui wa kila mtu, huwezi kufanikisha jambo la maana kwako bila kutumia pesa hapa ndipo tunavyoweza kuona adui huyu alivyo ingia katika ngazi ya soka.
Tumeshuhudia rekodi zikiweka na kuvunja katika kila msimu mpya wa ligi barani ulaya.Tulianza kuona rekodi aliyoweka Cristiano Ronaldo kutoka Manchester United kwenda Real Madrid,Real Madrid walito Pauni 80 Milioni wakamchukua Ronaldo hapo hapo miaka minne mitano ijayo Madrid hawa hawa walivunja rekodi ya mchezaji wao Ronaldo mara baada tu ya kumsajili Gareth Bale kwa pauni 86 milioni akitokea Tottenham Spurs. Hapa ndipo tunavyozidi kuona adui pesa alivyo jikita zaidi katika ulimwengu wa soka.
Leo hii Mchezaji aliyekulia katika klabu ya Manchester United akiwa tangu ana umri wa miaka 12 akaja kuuzwa na kuelekea Juventus akiwa na miaka 18 hivi sasa Manchester United hawa hawa wame mrudisha kwa pesa ya mwenda wa zimu ambayo ukifikiria haraka haraka unaweza ukasema kwanini pesa hizi zisingetolewa msaada katika nchi zenye uhaba wa wakimbizi, Lakini klabu pamoja na mawakala wa wachezaji hawajali hilo wao wanataka rekodi tu.
Paul Labile Pogba amejiunga rasmi na klabu ya Manchester United kwa rekodi ya aina yake,kwanza kabisa ameweza kuvunja rekodi ndani ya Manchester United pia amevunja rekodi ya dunia kwahiyo Ronaldo na Bale wapo chini yake yeye. Siku zote mawakala ndio watu wanaopiga pesa ndefu katika dili za wachezaji wakala wa Pogba Mino Raiola amekusanya mpunga wake mkubwa mno katika dili hili.
Habari zinasema kwamba Pogba amejiunga na Manchester United kwa ada ya Pauni 89 Milion na kuvunja rekodi ya dunia, vile vile Pogba ameweza kuwa mchezaji wa kwanza kuchukuliwa na Man United kwa ada kubwa kama hii ameweza kuwapita wachezaji hawa ambao nak pia walijiunga kwa pesa kubwa katika klabu ya Manchester United.
WACHEZAJI WALIOJIUNGA NA MANCHESTER UNITED KWA PESA NDEFU
5.Dimitar Berbatov- £ 30.7Ml
4.Anthony Martial- £ 36Ml
3.Juan Mata- £ 37.1Ml
2.Angel Di Maria- £ 59.7Ml
1.Paul Pogba- £ 89Ml
No comments:
Post a Comment