Hii ni Blog ya michezo ambayo inahusu sana mchezo wa soka, Hapa utaweza kupata habari mbalimbali za Soka katika kila sehemu duniani. Tangaza nasi kupitia 0713875490/0625557298
Hii ni Blog ya michezo ambayo inahusu sana mchezo wa soka, Hapa utaweza kupata habari mbalimbali za Soka katika kila sehemu duniani. Tangaza nasi kupitia 0713875490/0625557298
Pages
▼
Tuesday, August 9, 2016
ANTONIO CONTE ANAFAHAMU KAMA YUPO MIKONONI MWA ABRAMOVICH!?
Na: Ayoub Hinjo
Yuko wapi aliyesema tabasamu linaficha vitu vingi!? Maana pia kuna aliyesema aisifuye mvua imemnyea. Moyo huficha siri ambazo kwa macho huzioni sasa hili kuficha maumivu ya moyo tabasamu linatumika.
Ushawahi kuliona tabasamu la Roman Abramovich wakati Chelsea imepoteza mchezo!? Tabasamu lile limebeba maumivu ya moyo ambayo yanamfanya kuwaza mambo mengi sana hasa akitazama uwekezaji ambao ameufanya pale darajani.
Tabasamu la Roman linageuka mkuki ambao umeshawachoma makocha zaidi ya 6. Carlo Ancelloti alikumbana nao licha ya kuwapa makombe mawili timu hiyo. Jose Mourinho amejeruhiwa mara mbili nao huo licha ya kuwapa makombe pia. Sio hao tu hata aliyeipa Chelsea kombe la historia Di Matteo alifia kwenye mkuki huo.
Sasa Antonio Conte amevaa gwanda la ujenzi wa daraja jipya ambalo lilibomoka msimu ulioisha. Hakuna asiyejua kuhusu Chelsea ya mwaka jana ambayo ilimaliza nafasi ya 9 licha ya kuwa na wachezaji wengi wenye vipaji. Conte ni shujaa wa Juventus na Italia ambazo ameziongoza kwa mafanikio sana sana Juventus. Conte anakuwa shujaa kama Mourinho wakati anatoka Porto vivyo hivyo kwa Villa Boas.
Mkuki wa Roman Abramovich unaweza pita mbali na Conte kama atafanikiwa kumpa kile anachohitaji kwa kubeba makombe. Lakini sijui kama Conte anamjua Roman vizuri asijekupagawa na tabasamu lenye maumivu makali ya moyo.
No comments:
Post a Comment