Pages

Wednesday, August 10, 2016

RUVU SHOOTING,AFRICAN LYON NA MBAO FC MMEJIPANGA!?


Na: Ayoub Hinjo

Tarehe 20 Agosti itakuwa siku ambayo Ligi kuu ya Tanzania bara inaanza. Ligi kuu ya msimu huu tutaziona timu ambazo zimepanda daraja kuchukua nafasi za timu ambazo zimeshuka. Timu zilizopanda msimu huu ni Ruvu Shooting,African Lyon na Mbao FC na zilizoshuka ni Coastal Union,Mgambo JKT na African Sports zote za Tanga.

Mara nyingi maisha ya Ligi kuu yanakuwa magumu kwa timu zimepanda daraja kutokana na mfumo ambao wanakuja kukutana nao. Timu nyingi za madaraja ya chini zimekuwa zikicheza kwa kusimama kulingana na ratiba ambayo ipo,unaweza kuona timu inacheza mechi mbili ndani ya mwezi mmoja tofauti na ligi kuu ambayo kila wikiendi.

Udhaifu na ugeni kwenye ligi unaweza kuchangia kwa timu hizo kufanya vibaya. Sio timu zote zilizopanda daraja huwa zinashuka msimu huo huo zingine zinakuwa zimejipanga kama Mbeya City walivyofanya na timu zingine nyingi tu.

Ruvu Shooting,African Lyon na Mbao FC na imani hawatotaka kuwa daraja za timu kuchukulia ubingwa kupitia kwao na hiyo yote inawezekana kama watakuwa wamejipanga kwa mashindano na malengo yao kutimia.

No comments:

Post a Comment