Hii ni Blog ya michezo ambayo inahusu sana mchezo wa soka, Hapa utaweza kupata habari mbalimbali za Soka katika kila sehemu duniani. Tangaza nasi kupitia 0713875490/0625557298
Hii ni Blog ya michezo ambayo inahusu sana mchezo wa soka, Hapa utaweza kupata habari mbalimbali za Soka katika kila sehemu duniani. Tangaza nasi kupitia 0713875490/0625557298
Pages
▼
Thursday, August 11, 2016
"THROWBACK DAY": UNAKIFAHAMU KIKOSI CHA DHAHABU KILICHO MPATIA WENGER TAJI LA LIGI KUU BILA KUFUNGWA?
Na: Daniel Fute
Rekodi zinawekwa ili zivunjwe lakini si rekodi zote unaweza kuvunja utahangaika hata miaka 100 lakini itashindikana tu. Rekodi ambayo waliweka Arsenal mwaka 2004 katika michuano ya ligi kuu ya England wapo wengi wanadhani kwamba rekodi hii imefanywa na Arsenal pekee tu,lakini ukijua kwamba hao Arsenal walikuwa wana nia ya kuvunja rekodi iliyowekwa na klabu moja kutoka pale England ambayo ilikuwa tishio sana miaka ya 1970 mpaka miaka ya 90 hivi klabu hii inajulikana kwa jina la Nottingham Forest.
Hivi sasa klabu hii imebakia na historia tu maana kila kitu kwao kimekwisha na sasa ipo ligi daraja la kwanza hapo nchini England. Nottingham Forest ndio klabu iliyoweza kuweka rekodi ya kucheza ligi msimu mzima bila kufungwa na kuchukua ubingwa wa ligi katika msimu wa 1977/1978, Sasa basi baada ya hapo ikapita miaka 26 mpaka mwaka 2004 ambapo klabu ya Arsenal ndio walikuwa watu wa kwanza katika ligi hiyo kuvunja rekodi iliyowekwa na klabu hiyo ya Nottingham Forest.
Lakini je unakifahamu kikosi ambacho mpaka kesho kocha wa Arsenal bwana Arsene Wenger atabaki nacho kikosi hiki katika kumbukumbu yake bila kusahau mchezaji hata mmoja ambao waliifanikisha Arsenal kuwa klabu ya aina yake katika mwaka huo wa 2004. Leo napenda tuwe wote kukifahamu kikosi hiki ambacho kilijulikana zaidi kwa jina la 'The Invincibles' kilichoipelekea Arsenal kutwaa taji la England bila kufungwa mchezo hata mmoja.
GOALKEEPER
•Jens Lehman
Katika msimu huo wa 2003/04 golikipa huyu aliweza kuisaidia kwa kiasi kikubwa klabu yake baada ya kucheza michezo 38 ndani ya klabu hiyo. Kipa huyu kwa sasa ana umri wa miaka 44 na ni raia wa Ujerumani.
DEFENDERS
•Ashley Cole
Kabla hajajiunga na Chelsea lakini ameweza kuwaachia neno kubwa sana mashabiki wa Arsenal pamoja na aliyekuwa kocha wake kipindi hicho Arsene Wenger. Aliweza kuitumikia Arsenal katika msimu wa 2003/04 kwa kucheza michezo 32, Pia beki huyu anayecheza nafasi ya kushoto ni raia wa England.
•Sol Campbell
Kwa sasa ana umri wa miaka 40 lakimi kazi aliyoweza kuifanya katika msimu wa 2004 ni ya kipekee sana kwa beki huyu wa kati,Alicheza michezo 35.
•Lauren
Ana umri wa miaka 37 mpaka sasa aliweza kuitumikia Arsenal katika nafasi ya Beki wa kulia katika kipindi chote cha msimu wa 2004 maana aliweza kuanza michezo 30.
•Kolo Toure
Ni raia wa Ivory Coast lakini uwezo wake katika kipindi chake kilikuwa imara sana tofauti na sasa, aliweza kukipiga katika kikosi cha Arsenal michezo 36 katika msimu huo.
MIDFIELDERS
•Patric Viera
Huenda ndio ilikuwa roho ya timu na ndio alikuwa mtu sahihi katika kikosi hicho maana yeye ndio alikuwa jicho kwa wachezaji wenzake baada ya kukabidhiwa unahodha. Mfaransa huyu aliyecheza katika nafasi ya Kiungo ya katikati aliweza kucheza michezo 29 katika msimu huo wa ligi.
•Robert Pires
Alionekana kama Mjapan hivi kwa kumtazama lakini ni Mfaransa ambae alikuwa kiungo katika nafasi ya kushoto, aliitumikia michezo 33 katika msimu huo wa mafanikio.
•Frederick Ljungberg
Ni mzaliwa wa Sweden aliyekuwa anadumu hasa katika nafasi yake ya Kiungo wa upande wa kulia katika kikosi cha Arsenal, Ljungberg aliweza kuanza michezo 27 katika msimi huo wa ubingwa.
•Gilberto Silva
Huyu nae alikuwa sababu kubwa ya kuimarisha Arsenal katika nafasi ya Kiungo, pia Mbrazil huyu alikuwa chachu sana ya Wenger kwa kipindi kile ukimuondoa Edu.Mbrazil huyu alianza jumla ya michezo 29 katika kipindi hicho.
FORWARDS
•Thierry Henry
Mfaransa aliyekuwa tishio duniani alifanya ubora kila sehemu aliyoenda baada ya kutoka Arsenal na kuacha rekodi nyingi juu yake. Huyu alikuwa mfungaji wa aina yake alikuwa katika kila mechi na ndio chachu ya Arsenal kuwa bingwa katika msimu wa 2004.
•Dennis Bergkamp
Ni Bergkamp na si Beckham huyu ni Muholanzi aliyecheza kwa mafanikio makubwa chini ya kocha Wenger na huenda nae alikuwa na magoli ya kideo mengi katika msimu ule wa 2004, Alicheza michezo 21 katika ligi kuu mwaka huo.
Pia wapo wengine ambao walikuwa changamoto pindi wakitokea katika benchi kama Edu,Sylvain Wiltord, Jose Antonio Reyes, Pascal Cygan na Gael Clichy.
TUKUTANE TENA WIKI IJAYO KATIKA MFULULIZO WA 'THROWBACK DAY'.
No comments:
Post a Comment